Mkunapaa
Mandhari
(Elekezwa kutoka Croton pseudopulchellus)
Mkunapaa | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Mkunapaa (Croton pseudopulchellus) ni kichaka au mti mdogo wa nusufamilia Crotonoideae katika familia Euphorbiaceae. Unatokea misitu mikavu na savana kavu katika Afrika ya Magharibi, ya Kati, ya Mashariki na ya Kusini.
Maelezo[1]
[hariri | hariri chanzo]Spishi hii ni kichaka au mti mdogo wa m 1-6. Gome lake ni la kukwaruza lenye rangi ya kahawia au kijivu iliyofifia. Majani ni kama duaradufu, msingi kama kabari au labda kama mviringo, ncha butu au kali, upande wa chini wenye rangi ya fedha, mm 2.5-8.5 x 1-3.3. Maua ni meupe yenye urefu wa mm 3 na jinsia moja katika vishada vya mviringo. Matunda ni kijani-fedha yenye mabaka hudhurungi, umbo la ndewe tatu na kipenyo cha mm 6.
Matumizi
[hariri | hariri chanzo]Mti huu ni muhimu kama malisho ya mifugo katika nchi nyingi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Beentje, H.J. (1994) Kenya trees, shrubs and lianas. National Museums of Kenya, Nairobi.